Tumesaini mkataba na Coastal Union wa kumnunua Lawi na pia tumesaini na Lameck Lawi mwenyewe mkataba wa kuja kuitumikia Simba SC kwa Miaka mitatu (3), na pande zote tatu zimepata haki yake, hadi kufikia hatua ya kumtangaza mchezaji ni kwamba tumejiridhisha kila kitu kipo sawa" - Ahmed Ally.
Kwa mujibu wa taarifa Simba SC kabla ya kumsajili Lameck Lawi walishapeleka ofa mbili na zote zilikataliwa Coastal Union, Coastal walikubali ofa ya mwisho ya Simba na biashara ikafanyika. Hadi June 10, Simba ilimaliza malipo yote ya gharama za usajili wa Lameck Lawi kwa Coastal.